Biriani Kuku
Inatolewa na Isha Mashauzi-Tamtam Foodpoint
Biriani Kuku ni chakula kinachopikwa kwa mchanganyiko wa mchele na vipande vya kuku vilivyopikwa kwa viungo mbalimbali. Kuku huandaliwa kwa kupikwa katika mchuzi wenye vitunguu, nyanya, na viungo kama hiliki, karafuu, mdalasini na tangawizi. Mchele hupikwa kando au pamoja na mchuzi wa kuku, kisha vyote huwekwa kwa utaratibu ili kuleta mchanganyiko wa ladha na harufu nzuri