Vyumba vya Malazi
Inatolewa na Nyumbani Hotel
Nyumbani Hotel ina vyumba vya kisasa vya kulala vilivyowekwa kwa viwango vya hali ya juu. Kuna vyumba vya kawaida (standard), vya kati (deluxe), na vya kifahari (executive suites) vyenye huduma kama A/C, Wi-Fi, televisheni ya kisasa, maji ya moto, meza ya kazi, na huduma ya room service saa 24.