Vifurushi vya post paid bando/biashara
Huduma ya Vifurushi vya Postpaid kutoka Yas Tanzania imeundwa mahsusi kwa ajili ya kusaidia biashara na taasisi mbalimbali kupata huduma za mawasiliano . Kupitia vifurushi hivi, wateja hupata huduma za muda wa maongezi, ujumbe mfupi (SMS), na bando za intaneti, huku wakifanya malipo baada ya kutumia huduma hizo.
Bando za Muda wa maongezi
Bando za Muda wa Maongezi ni huduma inayotolewa na Yas Tanzania inayowawezesha wateja kupata dakika za kupiga simu kwa bei iliyopangwa. Huduma hii inalenga kurahisisha mawasiliano kwa kutoa vifurushi vya muda wa maongezi vinavyokidhi mahitaji mbalimbali ya wateja.
Vifurushi Vya Jumbe Fupi (SMS)
Bando za Ujumbe Mfupi (SMS) ni huduma inayotolewa na Yas Tanzania inayowawezesha wateja kutuma jumbe fupi za maandishi (SMS) kwenda ndani ya mtandao wa Yas au kwenda mitandao mingine nchini. Huduma hii inalenga kurahisisha mawasiliano kwa maandishi kwa kutoa vifurushi vya SMS vinavyokidhi mahitaji mbalimbali ya wateja.
Vifurushi vya Chuo
Vifurushi vya Chuo ni huduma maalum inayotolewa na Yas Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu. Huduma hii inalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na intaneti kwa wanafunzi, kwa kuzingatia mahitaji yao ya kiakademia na kijamii.
Mnunulie Rafiki
Hii ni huduma inayomuwezesha mtumiaji wa Ys Tanzania kununua vifurushi kwa ajiri ya rafiki anaetumia mtandao wa Yas au Mitandao Mingine. Mtumiaji anaweza kuhamisha salio au kununua kifurushi kwa rafiki, ndugu na jamaa
Vifurushi vya Internet/ Data
Hivi ni vifurushi vinavyomuwezesha mtumiaji wa Yas Tanzania kuweza kupata huduma ya kuperuzi mtandaoni
Huduma kwa wateja mix by yas
Huduma kwa Wateja ya Yas Tanzania ni mfumo wa msaada unaotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ili kuwasaidia katika masuala mbalimbali yanayohusiana na huduma zao. Kupitia huduma hii, wateja wanaweza kupata msaada wa kiufundi, taarifa kuhusu huduma, na usaidizi katika kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa matumizi ya huduma za Yas Tanzania.
Huduma ya Tigopesa/Mix by yas
Mixx by Yas ni huduma ya kifedha ya kidijitali inayotolewa na Yas Tanzania, ambayo awali ilijulikana kama Tigo Pesa. Huduma hii inawawezesha watumiaji kutuma na kupokea pesa, kulipa bili, kununua muda wa maongezi na vifurushi vya intaneti, pamoja na huduma nyingine za kifedha kupitia simu zao za mkononi au kwa kutumia programu ya Mixx by Yas.
Huduma za Mikopo ya fedha,Nivushe plus
Huduma hii inajumuisha mikopo midogo inayojulikana kama Nivushe Plus, pamoja na huduma nyingine kama Nipige Tafu na Bustisha, ambazo zinawalenga watumiaji wa kawaida na wafanyabiashara wadogo kuwapa uwezo wa kukopa na kulipa baadae kulingana na sheria na kanuni zilizowekwa.
Andika Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika maoniMtandao Tigo/YAS
YAS ni kampuni ya mtandao wa huduma za simu awali ilijulikana kwa chapa ya Tigo. Chapa ya YAS imeziduliwa rasmi tarehe 26 Novemba 2024. Kampuni hiyo wakati inaingia nchini Tanzania miaka takribani 30 iliopita ilianza kwa jina la Mobitel kabla ya kuitwa Tigo. Pia YAS imetangaza mabadiliko ya jina kwenye bidhaa yake ya TIGO PESA ambayo kuanzia leo itakuwa ikiitwa MIXX BY YAS. Hii sio mara ya kwanza kwa Kampuni hii kubadilishwa jina ilikuwa Mobitel (BUZZ), kisha TIGO na sasa ni YAS! Mabadiliko haya yametangazwa na Uongozi wa Kampuni hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo mchana ambayo Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa. Yas (iliyojulikana awali kama Tigo) ni kampuni ya mawasiliano ya mitandao ya simu nchini Tanzania.
Tovuti
http://www.tigo.co.tz
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 713123103