Ufuatiliaji na UKaguzi

Inatolewa na Ewura Head Office
0/5.0- Imepata 0 Maoni
Hakuna maoni ya kutosha. Acha maoni yako kuwasaidia wengine!

Ufuatiliaji na UKaguzi

Inatolewa na Ewura Head Office

EWURA hufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika taasisi, vituo, na mitambo mbalimbali ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa kwa wananchi zinazingatia viwango vya ubora, usalama, na ufanisi kama ilivyowekwa kisheria. Ukaguzi huu unahusisha maeneo mbalimbali kama: Kituo cha mafuta – EWURA hukagua vituo vya mafuta ili kuhakikisha bidhaa zinazouzwa zina ubora unaotakiwa, vipimo sahihi (kiasi cha mafuta kinachomwagwa hakikinzani na bei), na pia kuwepo kwa hatua za usalama kama vizima moto, alama za tahadhari, na usalama wa wateja. Mitambo ya uzalishaji na usambazaji wa umeme na maji – EWURA hukagua mitambo ya kuzalisha umeme (kama vile vituo vya gesi, hydro, au jua) pamoja na miundombinu ya kusambaza umeme na maji ili kuhakikisha kuwa inafanya kazi ipasavyo, haitoi madhara kwa mazingira, na inazingatia viwango vya kiufundi na usalama. Uzingatiaji wa viwango – Ukaguzi husaidia kuthibitisha kama taasisi au kampuni inayotoa huduma imezingatia masharti ya leseni, miongozo ya kiufundi, na viwango vya kitaifa au vya kimataifa vilivyowekwa.

Sign In