Huduma ya Uzazi na Afya ya Wanawake
Inatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Huduma hii inajumuisha kliniki za wajawazito, huduma za kujifungua, upasuaji wa uzazi, ushauri wa uzazi wa mpango, na matibabu ya matatizo ya mfumo wa uzazi. Wagonjwa hupata huduma kulingana na hatua ya ujauzito au tatizo la kiafya.