Huduma ya Mifupa (Orthopaedics)
Inatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Idara ya mifupa inahudumia wagonjwa wenye matatizo ya kuvunjika mifupa, maumivu ya viungo, ajali, na upasuaji wa kurekebisha mifupa. Pia kuna huduma ya tiba ya mazoezi (physiotherapy) kwa ajili ya kupona baada ya majeraha.