Huduma ya Macho (Ophthalmology)
Inatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Kliniki ya macho ya Muhimbili hufanya uchunguzi na matibabu ya matatizo ya macho kama presha ya macho, mtoto wa jicho, matatizo ya retina, na matatizo ya kuona. Pia hufanya upasuaji wa macho na kutoa miwani kulingana na hitaji la mgonjwa.