Usambazaji wa Bidhaa
Inatolewa na Azam Foods/Chakula
Azam Foods hutoa huduma ya usambazaji wa bidhaa zake katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Wana mtandao mpana wa usambazaji kupitia magari yao ya mizigo pamoja na mawakala walioko kwenye mikoa na nchi jirani. Bidhaa husambazwa kwenye maduka ya jumla, rejareja, supermarket, migahawa, hoteli, taasisi kama shule na hospitali.