Huduma ya Mikutano na Semina
Inatolewa na Kibo Palace Hotel
Hoteli inatoa kumbi za mikutano zilizopangiliwa kisasa kwa ajili ya vikao, semina, warsha, na makongamano. Kumbi hizo zina vifaa vya kisasa kama vile projectors, skrini kubwa, mfumo wa sauti wa hali ya juu, huduma ya intaneti ya kasi, viti vya kisasa na kiyoyozi. Pia, huduma ya chai, kahawa, chakula cha mchana na vitafunwa hutolewa kwa washiriki wa mikutano kulingana na mahitaji ya mteja. Huduma hii ni bora kwa mashirika, kampuni na taasisi zinazohitaji mahali pa kufanya mikutano ya hadhi ya juu.