Huduma za Kulazwa (Inpatient Care)
Inatolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Hospitali ina wodi tofauti kwa ajili ya wagonjwa wa kulazwa. Wodi hizo ni pamoja na wodi za wanawake, wanaume, watoto, wagonjwa mahututi (ICU), na wodi maalum kwa magonjwa kama saratani au matatizo ya akili.