Rating
Tags
Distance

Jaza energy-Nishati
Jaza Energy ni kampuni inayoshughulika na usambazaji wa umeme safi kwenye maeneo yasiyo na miundombinu ya gridi nchini Tanzania (na Nigeria)

Lake Oil Ltd
Lake Oil Ltd. (sehemu ya Lake Group) hufanya biashara na huduma zinazohusiana na mafuta na nishati nchini Tanzania na maeneo mengine East & Central Africa

Oryx Energies
Oryx Gas Tanzania Ltd ni kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa LPG (Liquefied Petroleum Gas) katika sehemu mbalimbali za Tanzania.

Total Energies
TotalEnergies ni kampuni ya kimataifa ya nishati ambayo inazalisha na kuuza vyanzo mbalimbali vya nishati, ikiwa ni pamoja na: mafuta na biofueli, gesi asilia na gesi ya kijani, renewables, na umeme.

Nkira Trading and Investment
Nkira Trading ni kampuni inayojihusisha na huduma za usafirishaji wa mizigo na ugavi. Wanatoa huduma mbalimbali zinazohusiana na mnyororo wa usambazaji wa bidhaa kutoka nje au ndani ya nchi

Work Nasi Hq
Worknasi ni kampuni ya kiteknolojia inayojikita katika ubunifu, teknolojia na huduma za TEHAMA. Kampuni hii inahudumia soko la Afrika na la kimataifa kwa kuunda na kutoa bidhaa pamoja na huduma za kiteknolojia kwa sekta mbalimbali.

Derm Elevators Limited
Derm Elevators Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania na inajihusisha na huduma za kiufundi katika sekta ya usafirishaji wa wima (vertical transportation), hasa kwa kutumia lifti na ngazi za umeme.

BF Suma
BF Suma ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za afya na lishe kwa matumizi ya binadamu.

Metl Group company
MeTL Group (Mohammed Enterprises Tanzania Limited) ni mojawapo ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na sekta mbalimbali za biashara na viwanda

Bakhresa Group
Bakhresa Group ni kundi la makampuni linalofanya kazi katika sekta mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.