King’amuzi (Decoder)
Dstv hutoa huduma ya ving'amuzi kama vile DStv HD Decoder na DStv Explora (PVR) – inayowezesha kurekodi na kuangalia vipindi baadaye.
Dish ya Satellite
DSTV wanatoa Dish ya satellite ambayo Hupokea mawimbi na kuonyesha channeli mbalimbali
Smart Card
Kadi ya kuwezesha usajili wa kifurushi na kufungulia maudhui.
App ya DStv Stream
Bidhaa ya kidigitali kwa ajili ya kutazama maudhui kwa njia ya mtandao.
Huduma ya Televisheni ya Kulipia kwa Satellite
Wateja hulipia kila mwezi ili kupata idadi ya chaneli kulingana na kifurushi walichochagua.
Vifurushi vya Chaneli vya Bei Tofauti
DStv Tanzania ina vifurushi kama vile: DStv Bomba DStv Access DStv Family DStv Compact DStv Compact Plus DStv Premium
Huduma ya Michezo Mubashara (SuperSport)
Inajumuisha mechi za Ligi Kuu England, La Liga, UEFA, NBA, Kriketi na michezo mingine ya kimataifa.
Huduma ya DStv Stream App
Wateja wanaweza kutazama vipindi kupitia simu janja, tablet au kompyuta, kwa kutumia akaunti yao iliyosajiliwa.
Huduma ya Ufungaji na Usanifu wa Vifaa
Mafundi wa DStv hutoa huduma ya kufunga na kusanifu king’amuzi, dish na vifaa vingine.
Huduma ya Malipo kwa Njia Mbali Mbali
Malipo ya kifurushi yanaweza kufanyika kwa M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa, benki, au mawakala waliopo nchini.
Huduma kwa Wateja
Kupitia simu, WhatsApp, mitandao ya kijamii, au ofisi zao, DStv hutoa msaada kwa masuala ya kiufundi au taarifa za kifurushi.
Kua wa kwanza Kutoa Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika Maoni YakoDstv Tanzania
DStv Tanzania ni huduma ya televisheni ya kulipia kupitia satellite, inayomilikiwa na kampuni ya Multichoice Tanzania. Inatoa chaneli mbalimbali za kitaifa na kimataifa katika vipengele vya habari, michezo, burudani, sinema, watoto, dini na tamthilia, kwa mfumo wa kulipia kila mwezi.
Tovuti
https://www.dstv.com/
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 659070707