Mafuta ya Kupikia (Azania Cooking Oil)Unga wa keki ya Azania kilo 25
Azania huzalisha mafuta ya kupikia kutoka kwenye mazao kama alizeti na mawese. Mafuta haya yanapatikana kwa ujazo tofauti – kuanzia pakiti ndogo za 500ml hadi madumu ya lita 20 – kwa matumizi ya nyumbani na biashara. Mafuta yao hupitia usafi wa hali ya juu na hupakiwa kwenye chupa au vipakio vilivyo salama kwa afya.
Unga wa Ngano (Azania Wheat Flour)
Azania huzalisha unga wa ngano kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya jikoni kama kupika chapati, maandazi, mikate, sambusa na keki. Unga huu hupatikana kwa vifungashio vya kilo 1, 2, 5 hadi 25, ukilenga watumiaji wa kawaida na wajasiriamali wanaoendesha biashara za chakula.
Tambi (Azania Spaghetti & Macaroni)
Azania hutoa Tambi spaghetti na macaroni zilizorahisi kupika. Bidhaa hizi hutumika majumbani na pia kwenye migahawa midogo na ya kati.
Mchele (Azania Rice)
Azania Group pia hufunga na kuuza mchele uliosafishwa tayari kwa kupikwa. Mchele huu hupatikana katika mifuko ya ujazo tofauti na ni sehemu ya bidhaa zao zinazolenga walaji wa kawaida na wa taasisi.
Unga wa Mahindi (Dona)
Azania Wanatoa Unga wa mahindi wa dona ambao hufaa kwa matumizi mbalimbali kulingana na mahitaji ya wateja
Unga wa Mahindi (Sembe)
Azania Group Linatoa Unga wa Mahindi wa sembe ambao unafaa kwa matumizi mbalimbali kulingana na mahitaji ya mteja
Usambazaji wa Bidhaa
Azania Group inatoa huduma ya usambazaji wa bidhaa zake kupitia mtandao wa mawakala, wauzaji wa jumla na magari yao ya usambazaji. Bidhaa zao zinafika kwenye supermarket, maduka ya rejareja, migahawa, taasisi kama shule na hospitali, na kwenye masoko ya kikanda.
Mauzo ya Jumla na Reja Reja
Kampuni huuza bidhaa zake kwa mfumo wa jumla kwa wauzaji wakubwa pamoja na reja reja kwa watumiaji binafsi. Hii inawapa nafasi wafanyabiashara na walaji wa kawaida kupata bidhaa kwa kiwango kinachowafaa.
Kua wa kwanza Kutoa Maoni Yako
Andika Maoni yako ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu biashara hii
Andika Maoni YakoAzania Group
Azania Group ni kampuni ya kitanzania inayojihusisha na uzalishaji, usindikaji, na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za chakula na bidhaa za viwandani. Ni moja kati ya makampuni ya ndani yaliyojijengea jina kutokana na ubora wa bidhaa na uwezo wa kuwafikia wateja wengi ndani ya nchi na ukanda wa Afrika Mashariki. Makao makuu ya Azania Group yapo Dar es Salaam, Tanzania.
Tovuti
https://azaniagroup.company/
Barua pepe
[email protected]
Simu
+255 710111112